Mhubiri Mlango 10 Ecclesiastes

Mhubiri 10:1 Ecclesiastes 10:1

Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.

Mhubiri 10:2 Ecclesiastes 10:2

Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kuume; Bali moyo wake mpumbavu upo mkono wa kushoto.

Mhubiri 10:3 Ecclesiastes 10:3

Naam, huyo mpumbavu tena, aendapo njiani, hupungukiwa na fahamu zake; hata humwambia kila mtu ya kuwa yeye ni mpumbavu.

Mhubiri 10:4 Ecclesiastes 10:4

Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.

Mhubiri 10:5 Ecclesiastes 10:5

Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye;

Mhubiri 10:6 Ecclesiastes 10:6

ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.

Mhubiri 10:7 Ecclesiastes 10:7

Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.

Mhubiri 10:8 Ecclesiastes 10:8

Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.

Mhubiri 10:9 Ecclesiastes 10:9

Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.

Mhubiri 10:10 Ecclesiastes 10:10

Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa.

Mhubiri 10:11 Ecclesiastes 10:11

Nyoka akiuma asijatumbuizwa, Basi hakuna faida ya mtumbuizi.

Mhubiri 10:12 Ecclesiastes 10:12

Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.

Mhubiri 10:13 Ecclesiastes 10:13

Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.

Mhubiri 10:14 Ecclesiastes 10:14

Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?

Mhubiri 10:15 Ecclesiastes 10:15

Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.

Mhubiri 10:16 Ecclesiastes 10:16

Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana, Na wakuu wako hula asubuhi!

Mhubiri 10:17 Ecclesiastes 10:17

Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu, wala si kwa ajili ya ulevi.

Mhubiri 10:18 Ecclesiastes 10:18

Kwa sababu ya uvivu paa hunepa; Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.

Mhubiri 10:19 Ecclesiastes 10:19

Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.

Mhubiri 10:20 Ecclesiastes 10:20

Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako; Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako; Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari.